14 Aprili 2012 - 19:30

ABNA inatuarifu kuwa:hatima ya kikako baina ya Jamhuri ya kiislamu ya Iran na kundi la 5+1 imepitisha na kukubali haki ya jamhuri ya kiislamu ya Iran ya kutumia teknolojia ya nyuklia kwa njia ya amani.

katika kikao hicho kilichofanyika jijini Istanbul Uturuki,Jamhuri ya kiislamuya Iran ilisisitiza umuhimu wake wa matumizi ya teknolojia hiyo kwa matumizi ya amani,pia ili elezea kuwa inapinga matumizi ya teknolojia hiyo kwa njia zisizo halali na inaomba mataifa yote yenye silaha za maangamizi yaharibu silaha zao ili kutimiza mpango wa amani duniani.

yafaa kuashiria kuwa Marekani na waitifaki wake wamekuwa wakiishinikiza jamhuri ya kiislam ya Iran kuachana na mpango wake wa nyuklia wa njia ya amani,ambapo waliahidi kuizuia kwa kadri ya uwezo wao na hatimaye kuiwekea vikwazo kadha wa kadha, nayo Jamhuri ya kiislamu ya Iran ilitoa radiamali kwa kuacha kuuza mafuta yake kwa baadhi ya nchi hizo jambo lilopelekea kupanda pei za mafuta duniani